Serikali imewatoa hofu watumishi
wote wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), na Shirika la Reli
Tanzania (TRL), kwa kuwahakikishia kuwa ajira zao hazitaathirika kwa
kuwa sheria mpya ya Reli ya Mwaka 2017 imeweka utaratibu maalum kwa
watumishi hao kuhamia kwenye taasisi mpya ya Kampuni ya Reli Tanzania
(TRC).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho
amesema hayo katika mahojiano maalum mjini Dodoma na kusisitiza taratibu
zote za kiutumishi zitafuatwa kwa watumishi watakoendelea na kazi
kwenye kampuni mpya.
“Sheria mpya ya reli mwaka 2017
imezigatia maslahi ya watumishi kwa kuweka mazingira mazuri kwa
wafanyakzi wa RAHCO na TRL hivyo atakaetaka kuendelea kutumikia umma
katika shirika hili jipya ataendelea na kazi na atakaetaka kucha kazi
basi taratibu za kiutumishi zitafuatwa kwa mujibu wa taratibu na Kanuni”
amesema Dkt. Chamuriho.
Dkt. Chamuriho amesema kuwa lengo
la kuunganisha taasisi hizo ni kuongeza ufanisi wa shirika hasa kwenye
usaifirishaji wa mizigo na kuondoa tofauti zilizokuepo kati ya RAHCO na
TRL ambazo zimekuepo kwa muda mrefu kwenye usimamizi na uendeshaji wa
shirika hilo.
Kwa upande wa Reli ya Kisasa (SGR)
Dkt. Chamuriho amesema kuanzishwa kwa sheria mpya kutaongeza ufanisi wa
utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya kwanza ambayo inahusisha awamu
tano ambapo awamu ya kwanza itajengwa kuanzia Dar es Salaam- Morogoro,
Awamu ya pili Morogoro-Makutupora, awamu ya tatu Makutupora-Tabora,
awamu ya nne Tabora-Isaka na awamu ya tano Isaka-Mwanza.
Aidha ameongeza kuwa baada ya
awamu hizo kukamilika Serikali itaanza awamu ya pili itakayohusisha
sehemu za Tabora-Kigoma, Mpanda-Kaliua na Ruvu-Tanga-Moshi-Arusha.
Kupitishwa kwa Sheria ya Reli ya
mwaka 2017 na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kunaifuta sheria
ya Reli No. 4 ya mwaka 2002 na sheria hii itaanza kutumika baada ya Rais
wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuisaini.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment