Monday, 20 June 2016

Serikali yaanza kufanya utafiti wa Picha zinazopigwa na ndege isiyo na rubani

indexPicha ya Angani zilizopigwa na Ndege Isiyo na Rubani (Drone) ambazo zinaaminika kuwa ni bora zaidi ya zile za awali.
Serikali imeanza hatua za awali za kufanyia utafiti wa ubora wa picha zinazopigwa na ndege isiyo na rubani katika matumizi ya kuandaa ramani.
 
Hadi sasa picha zilizopigwa zinaonyesha kuwa nzuri ambapo mafunzo zaidi juu ya matumizi ya picha hizo na jinsi ya kuandaa ramani yanahitajika.
Serikali ya Tanzania na ile ya Korea Kusini zinaendelea na mazungumzo ili Korea iweze kutoa mafunzo na ushauri wa kitaalam kuhusu matumizi ya drones katika kuchora ramani na kuhuisha ramani za siku nyingi.
Kwa kuanzia utaangaliwa uwezekano wa picha hizo kutumiwa kupanga ukuaji wa miji midogo kama Kibaigwa, Uvinza, Chanika na mingineyo ili ikue kimpangilio.

No comments:

Post a Comment