Wednesday 29 June 2016

Al Ahly kama Yanga, yadundwa kwa mara ya pili CAF

Klabu ya soka ya Al Ahly nayo ipo mashakani kutinga hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kukubali kipigo cha pili mfululizo ambapo jana walifungwa nyumbani mabao mawili kwa moja dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.
Wababe hao wa klabu ya Yanga walitangulia kupata bao la mapema likifungwa na Yannick Krahire Zakri dakika ya 29 lakini kipindi cha pili mambo yakabadilika na kushuhudiwa Mimosas wakasawazisha kupitia bao la kujifunga la Ahmed Hegazy naye Armand Niamke akaandika bao la pili.
Hapo awali Ahly walifungwa mabao matatu kwa mawili na Zesco United ya Zambia na sasa itahitaji ianze kuvuna matokeo mazuri katika mechi ijayo dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco.
Huo ni ushindi wa kwanza kwa Asec unaowapa alama tatu muhimu na kusawazisha makosa waliyoyafanya katika mchezo wa kwanza waliponyukwa na Wydad Casablanca bao moja kwa sifuri.
Hii leo Mchezo wa kundi hilo la A utazikutanisha klabu za Zesco United ya Zambia itakayoumana na Wydad Casablanca
.

No comments:

Post a Comment