Monday 27 June 2016

Nay wa Mitego kutambulisha wasanii wake

Nay wa Mitego.
 Msanii Nay wa Mitego ambaye siku si nyingi anatarajia kuachia kazi yake mpya 'Pale kati patamu' amesema kuwa baada ya kazi yake hiyo kutoka itakuwa ni wakati sahihi yeye kutambulisha rasmi wasanii walio chini ya Label yake ya 'Free Nation 966'.


Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live, Nay wa Mitego alisema kuwa yeye ni msanii wa kwanza kabisa kuanza kusimamia wasanii wenzake, na sasa ameona awatambulishe wasanii walio chini ya Label yake, ili afanye biashara ya muziki na siki kitu kingine.

"Unajua mimi ni msanii wa kwanza kuanza kusimamia wasanii wenzangu, mpaka sasa nina wasanii watatu ambao wapo chini ya Free Nation, lakini kwa kuanza tutaanza na mmoja ambaye tushakamilisha naye kila kitu anaitwa Tiki, nadhani Label yangu itakuwa na utofauti na Label nyingi sababu moja mimi ni mfanyabiashara hivyo hata msanii naye mleta lazima anaiingizie pesa huku akiwakonga mashabiki zake kwa muziki mzuri" alisema Nay wa Mitego.

Hivyo tutaanza na Tiki huku tukiangalia biashara yake inakwendaje, mimi sitaki kukurupuka nataka kufanya biashara, hivyo baada ya kazi yangu kutoka haitachukua muda atakuja Tiki kwa watanzania, ingawa chini Free Nation kuna wasanii watatu mpaka sasa" alisisitiza Nay wa Mitego.

No comments:

Post a Comment