Sunday 26 June 2016

Scotland kuzuia Uingereza kuondoka EU

 
Waziri Kiongozi wa Uskochi, Nicola Sturgeon, anasema bunge la Scotland linaweza kupiga kura kuzuwia Uingereza kutoka katika Umoja wa Ulaya.

Ali-iambia BBC anaamini, kikatiba, Uskochi lazima itoe idhini piya, kwamba Uingereza inaweza kumaliza uanachama wake katika EU na yeye atawasihi wabunge wa Scotland kutumia haki yao hiyo.
Uskochi ilipiga kura kwa wingi kubaki katika umoja huo
Bibi Sturgeon alisema, anataka kuwalinda watu wa Scotland na matokeo mabaya na ambayo yatawaumiza, nchi itapotoka katika Umoja wa Ulaya
Ameshazungumza juu ya uwezekano wa kufanya kura nyengine ya maoni, kujitenga na Uingereza.

No comments:

Post a Comment