Monday, 20 June 2016

Wastara Aamua Kuachana na Uigizaji

  Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amejipanga kuachana na uigizaji na kufanya ishu nyingine ikiwa ni pamoja na biashara ambazo ameanza kuzifanya.

Wastara alisema kuwa anamalizia kazi ya uigizaji mwaka huu na mwaka unaokuja atakuwa mwingine kabisa kwani baada ya kufika nchini Msumbiji (aliko kwa sasa) amepata dili lingine zuri ambalo ataliweka wazi baada ya mipango yake  kukamilika.
“Kinacho niachisha uigizaji si biashara tu bali ni pamoja na dili nililolipata huku Msumbiji, kama litakwenda nilivyopanga, nitaliweka wazi inshallah,” alisema Wastara.

Hivi karibuni, Wastara aliripotiwa kuwa na ujauzito ambapo alikimbilia nchini Msumbiji.

No comments:

Post a Comment