Kamati ya Olimpiki duniani IOC
inatarajiwa kujadili kauli tata la Urusi kupigwa marufuku kushiriki
mashindano yeyote ya riadha duniani na shirikisho la riadha duniani
IAAF.
Wandani wanatarajia kamati hiyo ya Olimpiki ambayo kimsingi
ndiyo inayoendesha michezo ya Olimpiki kuratibu kauli hiyo ya IAAF dhidi
ya wanariadha wa Urusi.Juma lililopita IAAF ilikataa kuondoa marufuku dhidi ya wanariadha wa Urusi ikisisitiza kuwa serikali ya nchi hiyo imekuwa ikiendesha mpango unaohujumu juhudi za shirika la kupambana na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini WADA za kubaini kiini hasa cha idadi kubwa ya wanariadha kutoka Urusi kupatikana na hatia ya kutumia madawa hayo haramu.
Wanariadha hao wanatuhumiwa kutumia madawa za kuongeza nguvu mwilini.
Kamati hiyo ya Olimpiki hata hivyo ina uwezo wa kubatilisha uamuzi wa IAAF uliokashifiwa na rais wa Urusi Vladimir Putin kuwa haikuwa ya haki haswa kwa wanariadha wa Urusi ambao hawajawahi kupatikana na hatia hiyo.
Aidha mbinu ya kukabiliana na mataifa mengine yaliyokiuka kanuni za WADA kama vile Kenya pia itajadiliwa.
No comments:
Post a Comment