Thursday 30 June 2016

Zlatan Ibrahimovic akaribia kutua Man Utd

 Ibra
Mshambuliaji nyota kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovicn anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake kujiunga an Manchester United wiki hii.
Mchezaji huyo wa umri wa miaka 34, kwa sasa hana mkataba na klabu yoyote baada yake kuondoka Paris St-Germain.


Anatarajiwa kutia saini mkataba wa mwaka mmoja Old Trafford.
Ibrahimovic atakuwa mchezaji wa pili kununuliwa na meneja mpya wa United Jose Mourinho, aliyemrithi Louis van Gaal mwezi Mei.
Beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 22, alikuwa wa kwanza kununuliwa.
United walilipa £30m kumchukua kutoka Villarreal ya Uhispania.
United pia wanaendelea kumuwinda Henrikh Mkhitaryan, 27, raia wa Armenia anayechezea klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
 
Ibrahimovic aliongoza ufungajji mabao Ligue 1 msimu uliopita, akifunga mabao 38.
Hata hivyo, hakuweza kufaa sana taifa lake la Sweden ambalo liliondolewa michuano ya Euro 2016 hatua ya makundi. Ibra hakufunga hata bao moja.

No comments:

Post a Comment