Thursday 30 June 2016

TP Mazembe kumnyakua mchezaji wa yanga Juma Mahadhi kwa gharma yoyote


 Na Kalonga Kasati
 
Moja ya kauli zilizotolewa na TP Mazembe walivyotua Tanzania kupambana na Yanga, ni kuwea mbali na mechi hiyo pia walipanga kuondoka na wachezaji wenye vipaji kutoka Tanzania kama walivyofanya kwa Mbwana Samatta.

Na baada ya mechi hiyo ya juzi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam na kuibuka na ushindi wa bao 1-0, jina la winga mpyawa Yanga, Juma Mahadhi, ndio lilinasa kwenye akili za mashabiki na mabosi wa Mazembe kama ilivyokuwa kwa Samatta mwaka 2011.


Kwa sababu uwezo alioonyesha juzi na Mahadhi ambaye alikua anacheza mechi yake ya kwanza akiwa na jezi ya Yanga, umewashawishi mashabiki na viongozi wa mazembekubeba jina la kinda huyo na kupania kulipeleka kwa tajiri wa klabu hiyo, Moise Katumbi. Inafahamika kuwa  Katumbi anawakubali na kuwaamini sana sana mashabiki wake na siku zote wakimpa jina la mchezaji huwa tayari  kuvunja benki kumsajili kama alivyofanya kwa Samattamiaka mitano iliyopita.

Katika mchezo wa juzi licha ya ugeni wake katika mechi kubwa za kimataifa, Mahadhi alionyesha kiwango cha hali ya juu na kuwa kuna watu walijitokeza kushuhudia pambano hilo na wengi wao wakaishia kusema tu kuwa kijana huyo hatadumu Jangwani kwa sababu watu watafika bei.

Kwa upande wake kocha wa yanga, Hans van der Pluijm, alionekana kukoshwa na kiwango cha kinda huyo na kumwagia sifa kemkem baada ya pambano hilo la pili la Yanga katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika.

"Nimefurahishwa na kiwango chake (Mahadhi), huu ni mchezo wake wa kwanza, lakini ameonyesha vitu vya hali ya juu uwanjani najivunia kuwa naye katika kikosi changu," alisema Pluijm.

Aliongeza licha ya uwanja wa Taifa kufurika mashabiki kibao lakini Mahadh alionyesha ukomavu wa hali ya juu na kuupiga mpira mwingi huku akiiweka katika wakati mgumu ngome ya TP Mazembe.

MAhadh alionekana kuwa na kasi na kutengeneza kona mbili ambazo hata hivyo hazikuzaa matunda kwenye mchezo huo ambao Yanga walilala kwa bao 1-0.

Hata hivyo katika dakika 65, Mahadhi aliumia na kushindwa kuendelea na pambano hilo na nafasi yake kuchukuliwa na Geofrey Mwashiuya.

No comments:

Post a Comment