Thursday 23 June 2016

Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji Charles Mwijage:amelitaka shirika la viwango Tanzania TBS pamoja na shirika la ushindani wa haki kuhakisha ifikapo July moja wanamaliza bidhaa zote bandia zinatoweka


Waziri wa Viwanda  Biashara na uwekezaji Charles Mwijage amelitaka shirika la viwango Tanzania TBS pamoja na shirika la ushindani wa haki kuhakisha ifikapo July moja  wanamaliza bidhaa zote bandia na  zilizo chini ya  viwango na wasipo fanya hivyo ajira zao zitafutwa mara na bidhaa hizo kuteketezwa.
 
Tamko hilo amelitoa waziri Charles Mwijage leo hii wakati alipokuwa anatembelea kujionea bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kusibitishwa ubora wake katika siku ya viwango afrika ambapo kwa upande wa kampuni ya cement ya Dangote afisa mkuu masoko Joel Laizer amemhakishi a waziri ubora wa cement zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Wakati huo huo kampuni ya Azania pamoja na Azam kwa kupitia kwa maofisa wao akiwemo Maofisa masoko  afisa mkuu wa masoko wa AZANIA  Naifa Abubakari pamoja Ibrahimu Masome wa AZAM  wamemuhakikishia waziri wa viwanda biashara na uwekezaji kuwa wao wamejipanga vizuri kuhakisha wanatoa bidhaa zinazokidhi viwango  bora na zenye ushindani na masoko kote duniani
Aidha kwa upande wao kampuni ya kuzalisha Bodi za magari ya kitalii pamoja na vyuma vya kujengea Maghala ya viwanda afisa biashara Mohan Krishan amemwambia waziri kuwa wao kama kampuni ya HANSPAUL  wataakikisha wanatengeneza bidhaa bora zenye bei nafuu.

No comments:

Post a Comment