Wales ilijifurukuta na kuilaza Urusi mabao matatu kwa nunge katika mechi ya mwisho na muhimu ya makundi jana usiku.
Aaron Ramsey na Neil Taylor na Gareth Bale walifunga mabao hayo muhimu na kuisaidia timu hiyo ya kocha Chris Coleman ikiwa imejihakikishia nafasi katika mkumbo wa pili kwa mara ya pili katika historia yake.
Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Wales sasa watachuana na mshindi wa tatu katika kundi C A ama D.
Vijana wa Chris Coleman wamewabamiza Russia mabao 3 kwa 0 na huku England ikija ya pili kwenye kundi baada ya kubanwa mbavu na Slovakia.
No comments:
Post a Comment