Shirika la Umoja wa mataifa
linalowashughulikia wakimbizi, UNHCR linasema kuwa idadi ya watu ambao
wameondolewa makwao kwa sababu ya mizozo, imepanda maradufu kuliko
wakati mwingine ule.
Katika ripoti yake ya kila mwaka inayohusiana
na rekodi ya watu wanaofurushwa makwao- UNHCR inasema kwamba, kufikia
mwishoni mwa mwaka jana, zaidi ya watu milioni 65 kote duniani, au mtu
mmoja kati ya 113 katika sayari hii ni mkimbizi, mhamiaji au
wakimbizi wa ndani kwa ndani.Zaidi ya nusu ya wakimbizi hao wote wanatoka nchini Syria, Afghanistan na Somalia.
No comments:
Post a Comment