Thursday 30 June 2016

Mwandishi wa ''The Concubine'' afariki

Elechi Amadi

Mwandishi maarufu wa Nigeria Elechi Amadi amefariki akiwa na umri wa miaka 82.
Amadi ambaye aliandika vitabu maarufu kama vile The Concubine,Isiburu,Sunset in Biafra,Peppersoup na The Road to Ibadan alifariki siku ya Jumatano mwendo wa saa tisa,wiki moja baada ya kuripotiwa kuugua.
Duru zimearifu kuwa marehemu alitarajiwa kuhudhuria hafla ya kusoma vitabu katika bandari ya Hacourt lakini hakuweza kutokana na kuugua kwake.

Akiwa mzaliwa wa eneo la Aluu katika jimbo la Riverstate mwaka 1934,Elecchi Amadi alisoma katika taasis ya Umuahia,Oyo na chuo kikuu cha Ibadan ambapo alipata shahada yake katika somo la fizikia na hesabati.

Pia aliwahi kufanya kazi kama mpimaji wa mashamba

No comments:

Post a Comment