
N’Golo Kante amesema kwamba mchezaji mwenzake Eden Hazard ndiye
anayestahili kuwa mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka England.
Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ubelgiji alifunga mabao yote wakati
timu hiyo ilipoilaza Manchester City mabao 2-1 mchezo uliopigwa katikati
ya wiki hii na kuwafanikisha kuongeza wigo wa pointi dhidi ya timu
inayoifuatia na kufikia pointi saba.
Kante ni miongoni mwa wachezaji nyota ambao wamekuwa wakitajwa kunyakua
tuzo hiyo msimu huu na amefanikiwa kujijenga tangu alipokuwa Leicester
City alipoiwezesha kunyakua taji msimu uliopita. Hata hivyo amekuwa
akisisitiza kwamba anayestahili tuzo hiyo ni kiungo wa Ufaransa, Hazard.
“Kwangu ni rahisi kumtaja mchezaji mwenzangu kutoka Chelsea. Wote
tumekuwa tukimuona Hazard anachokifanya. Ni mchezaji wa tofauti sana,”
alisema Cante alipokuwa akizungumza na mtandao wa Sky Sport.
Chelsea imekuwa katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England kwa mara ya
pili katika misimu mitatu. Nafasi yake kwa sasa ni kushinda michezo yote
sita iliyobaki na mchezaji huyo alisema kwamba wasiwaze kuhusu nafasi
ya pili inayoshikiliwa na Spurs.
“Bado tuna michezo nane na katika hiyo tunatakiwa kushinda mechi sita
tu. Tottenham ni timu nzuri na wanacheza mechi hizi ili nao watwae
ubingwa.”
“Kimahesabu tunahitajika kushinda mechi sita tu hivyo tunatakiwa
kujielekeza kwenye mioango yetu ya ushindi tukishinda mechi sita taji la
ubingwa tunalichukua mapema kabisa.”
No comments:
Post a Comment