Friday 21 April 2017

Hazard azungumzia ugomvi wake na Mourinho

Tangia Jose Mourinho aondoke Chelsea yamekuwa yakisemwa mengi, lakini ugomvi na wachezaji wakubwa wa Chelsea inaelezwa kama moja ya sababu ya Mourinho kuondoka Chelsea.
Kati ya wachezaji ambao inatajwa kama walikuwa na ugomvi na Mourinho ni Eden Hazard ambaye tetesi zinasema msimu wa mwisho wa Mourinho Chelsea waligombana sana na Hazard akawa hamsikilizi.
Baada ya uvumi huo kuenea kwa muda sasa, Hazard ameibuka na kuzungumzia ugomvi wake na Mou ambapo alikanusha na kusisitiza uhusiano wao ulikuwa mzuri sana na anamuheshimu sana kocha huyo.
“Tulikuwa na uhusiano mzuri tuu, kuna msimu nilikuwa mchezaji bora na ikamfanya atarajie makubwa kutoka kwangu msimu unaofuata ila mambo yakawa kombo, lakini nakumbuka uhusiano wangu na yeye ulikuwa mzuri sana” alisema Hazard.
Hazard anasema mahusiano yake na Mourinho yalikuwa mazuri kama ilivyo tu kati yake na kocha wa sasa wa timu hiyo Antonio Conte na kusema hakuwahi kuwa na tofauti yoyote na kocha huyo.
Hazard ambae tetesi zinadai yuko msimu wake wa mwisho Chelsea kabla ya kutimkia Real Madrid amesema Mourinho ni kocha aliyeshinda makombe kabla na baada ya Chelsea na ni lazima aheshimiwe kwa hilo.

No comments:

Post a Comment