Thursday 27 April 2017

Taifa la Venezuela lajiondoa muungano wa mataifa ya Marekani

Venezuela imetangaza kujiondoa kutoka kwa shirika la Umoja wa Mataifa ya Marekani Kusini OAS, ikidai mataifa ya jumuiya hiyo yanaingilia maswala ya ndani ya Venezuela.
Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bi Delcy Rodriguez ametoa kauli hiyo punde tu baada ya kikao cha jumuiya hiyo ya OAS kupiga kura ya kuitisha kikao maalum cha mawaziri wa mambo ya nje kujadili mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini humo.
Mataifa jirani ya Venezuela yameelezea wasiwasi wao kuhusu kuzorota kwa hali ya kisiasa na kiuchumi inayoendelea nchini humo.
Wakati huohuo mtu mwengine tena amefariki huko mjini Caracas katika maandamao ambayo yameikumba Venezuela kwa wiki ya tatu sasa yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 30.
Mtu huyo alifariki baada ya kugongwa na bomu la kutoa machozi lililorushwa na polisi waliokuwa wakijaribu kuwatawanya waandamanaji.
Waandamanaji hao wamekuwa wakimtaka rais wa nchi hiyo ajiuzulu kutokana kuzorota kwa uchumi wa nchi hiyo jambo lililosababisha upungufu mkubwa wa chakula.

No comments:

Post a Comment