Sunday 23 April 2017

Korea Kaskazini yamtia mbaroni raia wa Marekani

Shirika la habari la Korea Kusini linasema kwamba raia wa Marekani ametiwa mbaroni nchini Korea Kaskazini.
Bila kutaja vyanzo vyake, shirika hilo linasema mwanamume huyo mwenye asili ya kimarekani na kikorea alikamatwa akiwa kwenye uwanja wa ndege akijaribu kuondoka Pyongyang.
Inaarifiwa kwamba mwanamume huyo ni mhadhiri wa zamani wa chuo kikuu cha Yanbian Uchina, na alikuwa korea kaskazini kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa shughuli za uhisani.
Serikali za korea kusini na kaskazini hazijadhibitisha madai hayo.

Raia wengine wawili wa Marekani wanazuiliwa nchini humo.

No comments:

Post a Comment