Sunday 30 April 2017

Rais John Magufuli:' Napenda muniamini kuwa mimi nipo kwa niaba yenu, najua huu Urais si wangu

 
. Rais John Magufuli ameipa kwaya ya Jimbo Katoliki la Moshi, Parokia ya Kristo Mfalme, Sh1milioni ili irekodi nyimbo.
Pia imeipa kwaya ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri(KKKT) Usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro  Sh 1milioni ili kurekodi  nyimbo.
 Rais ametoa mchango wake huo leo aliposali katika makanisa hayo mjini Moshi na kuwaomba waumini wa makanisa hayo wamuoembee.
Rais Magufuli amesema hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano zina lengo la kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli ya taifa linalomuamini Mungu.

'' Napenda muniamini kuwa mimi nipo kwa niaba yenu, najua huu Urais si wangu, Urais mnao ninyi mlioamuwa nitumike kama mtumishi kwa wakati huu, nawaomba sana muendelee kuniweka katika sala zenu ili kazi hii ya Urais isinipe kiburi, nikawe mtumishi wa watu,” amesema

 Kadhalika Rais alitoa mifuko ya saruji kwa makanisa yote mawili ili kusaidia  ujenzi wa makanisa hayo

No comments:

Post a Comment