Friday 21 April 2017

Kaduguda:mpira wa miguu hapa nchini unaendeshwa na watu wasio na uelewa wa mchezo

Jamal+Malinzi
Aliyekuwa katibu mkuu wa klabu ya Simba,Mwina Kaduguda amesema kwamba kwa sasa mpira wa miguu hapa nchini unaendeshwa na watu wasio na uelewa wa mchezo huo ndio maana mara kwa mara kunaibuka migogoro ambayo haina msingi.
Kaduguda ameshangazwa na yanayoendelea hivi sasa juu ya sakata la mchezaji wa timu ya Kagera Sugar Mohamed Fakh aliyecheza mechi zidi ya Simba akiwa na kadi tatu za njano baada ya kubainika na kamati ya masaa 72.
Hata hivyo alisema kwamba migogoro hiyo haitaweza kuisha endapo kama viongozi wanaongoza mpira wataendelea kuwa walewale wa siku zote ambao kiuhalisia hawana hadhi ya kuongoza mpira wa miguu.

No comments:

Post a Comment