
Wahudumua wa ndege ya shirika la ndege la Uturuki, walisherehekea
kuwasili kwa abiria mwingine angani umbali ya futi 42,000 au mita
12,800, wakati mwanamke mmoja alijifungua mtoto msichana.
Abiria nao walisaidia kuzaliwa kwa mtoto huyo, muda mfupi baada ya ndege
hiyo kupaa kutoka mji mkuu wa Guinea, Conakry, ikielekea Isanbul
kupitia Burkina Faso.
Mama wa mtoto huyo aliyepewa jina Kadiju, walipelekwa hospitali wakati
ndege hiyo aina ya Boeng 737 ilipotua mji mkuu wa Burkina Faso,
Ouagadougou.

Wote waliripotiwa kuchoka lakini walikuwa na afya nzuri.
Wahudumu waligundua kuwa mwanamke mmoja abiria kwa jina Nafi Diaby, alikuwa akihisi uchungu wa kujifungua.
Hapo ndipo walichukua hatua ya kumsaidia kujifungua ndege ikiwa safarini.

Mashirika mengi ya ndege huruhusu mama walio wajawazito wa hadi wiki 36
kusafiri, lakini uhitaji barua ya daktari wakifikisha wiki 28 kuonyesha
tarehe wanayotarajia kujifungua.
No comments:
Post a Comment