Tuesday 25 April 2017

Faida za kula dagaa katika miili yetu

 No automatic alt text available.
Kwa imani watu wengi,
dagaa ni kitoweo cha kimaskini,
huonekana kua kununua dagaa
sokoni au ‘super market’ kwa
ajili ya kitoweo, ni dalili ya
muhusika kuishiwa au kua na
bajeti ndogo.
Tunapoangalia umuhimu wa
dagaa na faida zake katika mwili
wa binadamu,tunagu ndua kua
uwe maskini, tajiri au bilionea,
kama unajali afya yako, dagaa ni
muhimu kula kuliko
mapochopocho unayokula
kifahari.
Leo tutaangalia faida za kiafya
za dagaa, tunaambiwa kua wana
faida kubwa sana katika
kupambana na kutoa kinga ya
magonjwa hatari ya moyo!
FAIDA KWA AFYA YA MOYO
Kama ilivyo kwa karanga na
korosho,dagaa nao
wameonesha kua na faida
kubwa kwa wenye matatizo ya
magonjwaya moyo.
Dagaa wana virutubisho vingi,
ambapo miongoni mwa
virutubisho hivyo kuna kiwango
kikikubwa cha Omega-3 Fatty
Acids (EPA & DHA).
Katika tafiti nyingi za magonjwa
ya moyo na tiba zake,
virutubisho vya Omega 3
vimeonekana kua ni dawa au
kinga kubwa sana ya magonjwa
ya moyo.
Chanzo kikuu cha virutubisho
hivyo ni samaki na dagaa.
Aidha, dagaa pia ni chanzo kizuri
cha Vitamin B12, ikiwa ni chanzo
kizuri cha pili baada ya maini.
Vitamin hii hufanya kazi kubwa
ya kuboresha ustawi wa moyo,
na hivyo kua chakula kizuri cha
kumpa ahueni au kinga
madhubuti mlaji dhidi ya
magonjwa ya moyo.
AFYA YA MIFUPA
Dagaa ni chanzo kingine kizuri
cha madini ya ‘Calcium’ yenye
jukumu la kuimarisha mifupa ya
mwili, lakini pia kwenye dagaa
kuna vitamin D ambayo hua
nadra sana kupatikana kwenye
lishe.
Vitamin D hufanyakazi muhimu
ya kuimarisha afya ya mifupa
kwani ndiyo inayosaidia
unyonywaji wa madini ya
‘calcium mwilini’.
Vile vile dagaa ni chanzo kizuri
cha madini aina ya ‘phosphorus’,
ambayo nayo huimarisha
mifupa.
Dagaa Dhidi ya Kansa
Kwa miaka mingi, watafiti
wameona jinsi ambavyo dagaa
wanavyoweza kudhibiti seli
zinazosambaza saratani mwilini.
Hivyo imethibitika pasi na shaka
kua virutubisho vilivyomo
kwenye dagaa, huweza kutoa
kinga kubwa dhidi ya ugonjwa
wa saratani.
Dagaa wana
Protini kubwa
Kama una upungufu wa protini
mwilini, basi kula dagaa, kwani
wao wana kiwango kikubwa
cha kirutubisho hicho.
Protini husaidia uzalishaji wa
‘Amino acids’ ambazo ni muhimu
kwa uzalishaji wa chembe hai
mwilini, na uimarishaji wa
mfumo wa kinga ya mwili (body
immune system).
kwa Dagaa safi na waliobora wasiliana na Ipyana Mwakamela kwa simu 0784300020 au 0713300020

No comments:

Post a Comment