Friday 21 April 2017

Paul Pogba, Ander Herrera waongoza kupiga pasi nyingi

Katika msimu huu wa ligi ya Uingereza manina ya viungo kama Paul Pogba, Ander Herrera, Ngolo Kante na Jordan Henderson wamekuwa wakizungumziwa sana kutokana na uwezo wao wa kupiga pasi.
Lakini takwimu zinaonesha anayeongoza kwa kupiga pasi zilizowafikia walengwa wala sio kiungo bali ni mlinzi, beki wa kulia wa Chelsea Cesar Azpilicueta ndio mchezaji anayeongoza kupiga pasi zilizowafikia walengwa.
Azpilicueta hajapiga pasi nyingi kama Pogba au Henderson lakini pasi zake chache alizopiga ziliwafikia walengwa na kumfanya kukamilisha pasi kwa 87.62%.
Azpilicueta amepiga pasi 2028 lakini kati ya hizo, pasi 1777 ziliwafikia walengwa na hiyo kumfanya kuwa na wastani huo wa 87.62%, huku kiungo wa Liverpool Jordan Henderson akiwa nafasi ya pili.
Henderson hadi sasa amepiga pasi 2057, ikiwa ni pasi nyingi kuliko Azpilicueta lakini katika pasi za Henderson ni pasi 1767 sawa na 85.90% ambazo zimewafikia walengwa.
Paul Pogba naye hadi sasa amepiga pasi nyingi zaidi kuliko Henderson na Azpilicueta ikiwa ni pasi 2070 lakini kati ya pasi hizo za Pogba ni jumla ya pasi 1763 tu zilizowafikia walengwa.
Ngolo Kante yuko nafasi ya nne chini ya Pogba akiwa amepiga pasi chache kuliko Pogba, Kante amepiga pasi 1899 lakini kati ya hizo ni pasi 1686 alizofanikiwa kufikisha kwa walengwa.
Ander Herrera wa Manchester Unite yuko nafasi ya tano ambapo hadi sasa amepiga pasi 1853, kati ya pasi hizo ni pasi 1629 ambazo Herrera alikamilisha.

No comments:

Post a Comment