Saturday 22 April 2017

Baba Levo airushia Dongo Chama Tawala

Image result for babalevo
Diwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini, Kigoma kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Baba Levo amesema wakati anakabidhiwa Zahanati ya kati hiyo ambayo ilikuwa chini ya CCM toka Tanzania inapata uhuru, ilikuwa na uwezo wa kupima Malaria na kupima uzito tu.
Akiongea kwenye kipindi cha East Africa Breakafast Baba Levo amesema kata hiyo ilikuwa haina maendeleo kutokana na kuwa chini ya CCM kwa muda mrefu lakini toka kata hiyo imechukuliwa na upinzani chini yake saizi imepiga hatua ndani ya muda mfupi.
"Kata ya Kigoma Kaskazini ilikuwa inaitwa Butiama kwa sababu toka nchi hii imezaliwa ilikuwa inaongozwa na CCM sasa shida moja iliyoikuta ile kata unakuta kiongozi anayeongoza ile kata ni CCM lakini Kigoma Mjini yenyewe mara nyingi ilikuwa inaongozwa na madiwani wa upinzani, kwa hiyo unajikuta ile Kata uwezo wa kupata maendeleo ni ngumu" alisema Baba Levo
Mbali na hilo Baba Levo anasema wakati anakabidhiwa Zahanati hiyo na CCM ilikuwa na uwezo wa kutibu Malaria tu na kupimisha uzito kwa watoto.
"Sasa hivi kata ya Mwanga Kaskazini imekuwa ndiyo bora kwa mkoa wa Kigoma, imekuwa bora kwa sababu diwani wao nimetimiza ahadi zangu maana mimi niliahidi ahadi saba tu, na kwa mwaka wangu wa fedha wa 2016/2017 nimetimiza ahadi tatu kwa hiyo katika miaka mingine iliyobakia natakiwa kutumiza ahadi nne ambazo ni rahisi tu. Mimi wakati naipokea ile kata nilikuta ina zahanati lakini zahanati ile ilikuwa inatibu Malaria peke yake, kumbuka Zahanati ina kiwango cha magonjwa ambayo inatakiwa itibu yakizidi mgonjwa aende hospitali kubwa lakini zahanati hiyo ilikuwa inatibu Malaria peke yake na kupima uzito watoto kama kliniki sasa nikajiuliza kama hii inahudumua watoto peke yake hii ni zahanati au Chekechea ya watoto? alihoja Bab Levo


Baba Levo anasema toka amekuwa diwani saizi hiyo zahanati imekuwa ikitoa huduma zote na kusema amezidi kuiboresha, kwa kuingiza maji, kufunga umeme, pamoja na kujenga vyoo vizuri.

No comments:

Post a Comment