Sunday 23 April 2017

Mashabiki wa Chelsea wampokea Drogba Marekani

 Mshambuliaji mkongwe, Didier Drogba amepokelewa kwa shangwe wakati akitua nchini Marekani kujiunga na timu ya Phoenix Rising ya mjini Arizona.
Lakini ajabu, mashabiki wengi wa Phoenix walionekana zaidi ni mashabiki wa Chelsea, timu ambayo Drogba alipata umaarufu mkubwa.
Mashabiki hao walitaka Drogba kusaini jezi za Chelsea ya England badala ya Phoenix ambayo ni timu yao.
Kilichovutia zaidi mashabiki hao walikuwa na jezi mpya zinazotumiwa sasa na Chelsea, zikiwemo zile za nyumbani na ugenini.
Drogba alipata mafanikio makubwa akiwa Chelsea ambako aliiongoza kubeba makombe lukuki kama Kombe la Ligi, Kombe la FA, Ubingwa wa England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.





No comments:

Post a Comment