Saturday 22 April 2017

Wanasaikolojia wasema Watu waliofikia elimu ya Chuo Kikuu hawapati magonjwa ya akili

Utafiti uliofanywa na Wanasaikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Exeter, Uingereza umegundua uhusiano uliopo baina ya elimu na magonjwa ya ikisemwa kuwa watu waliofika hatua ya Chuo Kikuu wana asilimia ndogo ya kupata magonjwa ya akili ukilinganisha na watu ambao hawakufikia kiwango hicho.
Utafiti huu ulihusisha watu zaidi ya 2,315 wenye umri wa miaka 65 ambapo zaidi ya nusu ambao hawakufika elimu ya Chuo Kikuu walionesha dalili za magonjwa ya akili kama Dementia na Alzheimer huku waliofika hatua hiyo wakionesha kutokuwa na dalili ya magonjwa hayo.
Profesa Linda Clare, Mtaalamu wa mambo ya ubongo alisema:“Mara nyingi watu wanaopata magonjwa ya akili wanapofikisha umri mkubwa ni watu ambao hawakupata elimu kubwa. Hii ni kwa sababu kupata elimu kunakusaidia kushughulisha akili. Hivyo ni vigumu kupatwa na magonjwa yanayoathiri ubongo.”

No comments:

Post a Comment