Saturday 22 April 2017

Mshauri mkuu wa kiongozi wa Taleban auawa na Marekani

Kiongozi wa kundi la Taleban Abu Bakr al -Bhagdad
Makao makuu ya jeshi ya Marekani, Pentagon, yamemlenga na kumwua mshauri mkuu wa kiongozi wa Taliban, Abu Bakr al -Bhagdadi katika shambulio lililofanywa nchini Syria.
Msemaji wa Pentagon, kanali John Thomas, alisema kuwa Abdul Rahman al-Uzbek, aliuawa Aprili 6 lakini hakutoa taarifa zaidi.
Alisema kuwa Al-Uzbeki alishiriki katika kupanga mashambulizi kwenye kilabu kimoja usiku wa kuamkia mwaka mpya mjini Istanbul ambako watu 30 walifariki.
Mwandishi wa BBC alisema kuwa ingawa kuna wanajeshi zaidi ya 500 wa Marekani kutoka kikosi maalumu nchini Syria kwa kawaida hawashiriki katika oparesheni moja kwa moja.

Alisema wao hutumia muda mwingi kutoa ushauri kwa makundi asilia ya maeneo hayo jinsi ya kukabiliana na wapiganaji wa Islamic State.

No comments:

Post a Comment