Tuesday 25 April 2017

Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita amefanya safari ya kikazi Nchini Iran

unnamed
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akipunga mkono kuaga wananchi wake wa jiji lake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam jana jioni tayari kwa safari kuelekea Nchini Iran kwa ziara ya kikazi ya siku kumi (10),akiwa nchini humo atakutana na Rais wa Iran, Hassan Rouhani,Mwenyeji wake,Meya wa Jiji la Teheran, Muhammed Bakir Galbaf na kushuhudia kampeni za uchaguzi mkuu zinazoendelea nchini humo.
NA CHRISTINA MWAGALA, OMJ
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ,ameondoka Nchini jana kuelekea Iran kwa mualiko wa ziara ya kikazi ya siku 10 ikiwemo na mkutano wa siku mbili  utakaofanyika katika mji wa Bashar.
Aidha Meya atapata nafasi ya kuzungumza na rais wa Jamhuri ya Kiislamu wa Iran Hassan Rouhani kabla ya kufanyika kwa mkutano wa siku mbili katika jiji la Bashar utakao husisha majadiliano mbalimbali kuhusu majiji.
Katika mkutano huo ambao utahusisha majadiliano mbalimbali kuhusu majiji, ambapo baada ya mkutano huo ataelekea mjini Teherani  kwa mualiko maalumu wa Meya wa jiji hilo Muhammed Bakir Galbaf ambapo pamoja na mambo mengine watajadiliana fursa za kibiashara katika majiji hayo mawilI.
Aidha katika mazungumzo hayo, watajadiliana pia namna ya kutatua changamoto zilizopo kwenye majiji na namna ambavyo wanaweza kuyatatua.
“ Iran na Tanzania ni nchi marafiki kwa kipindi kirefu kwahiyo utaona kwamba mambo mengi wamekuwa wakishirikiana na sisi, kwahiyo ni fursa pia kwa majiji haya mawili kubadilishana uwezo wa kuendeleza jiji letu, nimechaguliwa na wananchi na wao wanataka maendeleo “ alisema Meya Isaya.
 
Aliongeza kwamba akiwa nchini humo atapata fursa ya kushuhudia kampeni za uchaguzi mkuu ambapo miongoni mwa wagombea wa nafasi ya urais Meya wa jiji la Teheran ni mmoja wapo.
“ Kushudia kwangu kampeni sio kwamba nataka kugombea nafasi ya uras hapa nchini , hapana ila ni moja ya kujifunza namna ambavyo wenzetu wanafanya kampeni zao” alifafanua.
Hata hivyo Meya aliwasi wakazi wa jiji la Dar es Salaam hususani wanaoishi mabondeni kuchukua tahadhari kwani bado mvua zinaendelea kunyesha na hivyo kujikinga na mafuriko.

No comments:

Post a Comment