Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari za
Michezo Jijini Dar es Salaam alipokutana nao leo Jijini Dar es Salaam
wakati wa semina maalum iliyoandaliwa na Kampuni ya Selcom kujadili
kuhusu matumizi ya mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika
Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha waandishi wa
habari wa michezo Tanzania (TASWA) Bw. Juma Pinto akizungumza katika
semina maalum iliyoandaliwa na kampuni ya Selcom kwa ajili ya kujua
matumizi ya mfumo wa mashine za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa
Jijini dar es Salaam
Meneja wa Miradi kutoka kampuni
ya Selcom Bw. Galus Runyet akitoa maelezo kwa waandishi wa habari za
Michezo kuhusu matumizi ya mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki
katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Miradi kutoka kampuni
ya Selcome Bw. Galus Runyet akitoa maelezo kwa waandishi wa habari za
Michezo kuhusu jinsi ya kutumia kadi ya mfumo wa mashine za tiketi za
kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari za
Michezo wakimsililiza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye wakati wa semina maalum iliyoandaliwa na Kampuni ya
Selcom kujadili kuhusu matumizi ya mfumo wa mashine za tiketi za
kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Picha Zote na Raymond Mushumbusi WHUMS
No comments:
Post a Comment