Tuesday 27 September 2016

Clinton ambwaga Trump kwenye mdahalo


Hillary Clinton amembwaga mpinzani wake, Donald Trump kwenye mdahalo wao wa kwanza, uliofanyika Jumatatu jijini New York, Marekani.
Kwa mujibu wa kura za CNN/ORC, Clinton amepata asilimia 67 na Trump kuambulia asilimia 27 tu.
 Mahasimu hao wanaochuana kuingia White House, wametifuana kwenye ule unaoweza kuwa mdahalo wa Urais uliotazamwa zaidi katika historia ya Marekani.
Watu milioni 100 walitazamiwa kuangalia mdahalo huo wa kwanza kati ya Donald Trump wa chama cha Republican na Hillary Clinton wa chama cha Democratic.
 Wawili hao waliingia kwenye mdahalo katika kipindi ambacho kura za maoni zinawaonesha wakikaribiana kwa kiasi kikubwa. Kwenye mdahalo huo walizungumza kuhusu kazi, usalama, mwelekeo wa Marekani na mambo mengine.
Mdahalo huo ukaibua pia mambo yao binafsi kama vile Trump kugoma kuonesha rekodi zake za ulipaji kodi na kashfa ya Clinton kutumia barua binafsi enzi akiwa waziri wa mambo ya nje.

Trump alidai kuwa pindi Clinton akizionesha barua pepe 30,000 zilizopotea, yeye pia ataonesha rekodi za ulipaji kodi wake.
Clinton alimshambulia Trump kuwa ni mwepesi mno kughafikirishwa na hivyo hafai kuwa amri jeshi mkuu.
“A man who can be provoked by a tweet should not have his fingers anywhere near the nuclear codes,” alisema Clinton.

Wachambuzi wengi wa masuala ya siasa wanadai kuwa Clinton amefanya vyema kuliko Trump kwenye mdahalo huo. Wawili hao watakutana kwenye midahalo mingine miwili, October 9 na October 19.

No comments:

Post a Comment