Monday 26 September 2016

Ziara ya Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai kutembelea Baraza la Wawakilishi Zanzibar

spi1
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiwasili Mjini  Zanzibar kwa kutumia Boti wakati alipofanya ziara ya kutembelea Baraza la Wawakilishi mapema leo Septemba 2016.
spi2
Spika wa Bunge  Mhe Job Ndugai akisalimiana  na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (katikati)  alipowasili katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kushoto ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma.
spi3
Spika wa Bunge  Mhe Job Ndugai (kulia) akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (katikati) na Naibu Spika wa Baraza hilo  Mhe Mgeni Hassan Juma wakati alipowatembelea.
spi4
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa tatu toka kulia) akifuatilia kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati alipowatembelea. Wapili kulia ni Spika wa Baraza hilo Mhe Zuberi Ali Maulid na wa kwanza kulia ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma.
spi5
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai kiwasalimia Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar alipotambulishwa wakati wa kikao cha Baraza hilo.
spi6
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid (kulia) na Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe Mgeni Hassan Juma (kushoto).
spi7
Spika wa Baraza la Wawakilishi  Mhe Zuberi Ali Maulid akimuelezea jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai wakati wa ziara hiyo.
 Picha na Ofisi ya Bunge

No comments:

Post a Comment