Sunday 25 September 2016

Rais John Magufuli leo amesali katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano lililopo Posta jijini Dar es Salaam

 
Rais John Magufuli leo asubuhi ameungana na Waumini wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano lililopo Posta jijini Dar es Salaam kusali ibada ambapo amewashukuru viongozi na waumini wa kanisa hilo na madhehebu mengine ya dini hapa nchini kwa kuendelea kuliombea Taifa na kudumisha amani na utulivu. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa Rais Magufuli amesisitiza kuwa viongozi wa dini wanafanya kazi kubwa na muhimu katika Taifa na kwamba Watanzania wote bila kujali dini zao, itikadi za kisiasa, makundi na kanda zao wana wajibu wa kuungana na viongozi hao ili nia hiyo njema iendelee kufanikiw

No comments:

Post a Comment