Friday 30 September 2016

Nape amewatoa wasiwasi kuhusu upatikanaji wa tiketi kuelekea mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara kati ya watani wa Jadi Yanga na Simba

nna1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)  leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya matumizi ya tiketi za kieletroniki  kuelekea mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara ya watani wa Jadi Yanga na Simba itakayochezwa kesho Oktoba Mosi leo ,2016.
nna2
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya upatikanaji  wa tiketi za kieletroniki  kuelekea mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara ya watani wa Jadi  Yanga na Simba itakayochezwa kesho Oktoba Mosi leo ,2016 kushoto ni Meneja Mradi kutoka kampuni ya Selcom Tanzania Bw. Gallius Runyeta.
nna3
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akieleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya matumizi ya tiketi za kieletroniki  kuelekea mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara ya watani wa Jadi Yanga na Simba itakayochezwa kesho Oktoba Mosi leo ,2016 kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw. Alex Nkenyenge.
nna4
Waandishi wa Habari wakifatilia mkutano huo.
nna5
Waandishi wa Habari wakifatilia mkutano huo.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Mashabiki wa soka nchini wameondolewa wasiwasi kuhusu upatikanaji wa tiketi kuelekea mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara kati ya watani wa Jadi Yanga na Simba na kuhakikishiwa kuwa mfumo wa upatikanaji tiketi uko vizuri na mpaka sasa tiketi zinaendelea kuuzwa katika maeneo mbalimbali.
 Wasiwasi huo umetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu matumizi ya tiketi za kieletroniki kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba.
Waziri Nape amesema kuwa kuna kuna taarifa kutoka mitaani kuwa kuna uwezekano wa mfumo huu kutofanya kazi  katika mechi hii na malalamiko ya watu wengi  kulalamika kukosa tiketi za mchezo wa kesho.
 
“kwa kila anayetaka kwenda uwanjani kesho kadi zinapatikana nimewaagiza Selcom wahakikishe wanazungusha  magari  yao mtaani  kuangalia  mahali penye upungufu na  yawe na watu wenye kadi hizo aidha,  watu waongezwe kwenye vituo ambayo vina idadi kubwa ya wateja wanaohitaji kadi” Alisema Mhe Nnauye.
Aidha Waziri Nape Nnauye amewahakikishia watanzania kuwa atausimamia mfumo huu kikamilifu na kwa gharama yoyote na  atahakikisha  hautakuwa  na mapungufu na endapo  yatajotokeza yatashughulikiwa na wataalamu ili kuufanya mfumo huu kufanya kazi ipasavyo kama ulivyokusudiwa.
 Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka Selcom Tanzania Galius Runyeta  amefafanua kuwa mfumo huu uko wazi kabisa kwa wadau wote wanaohusika na mapato ya uwanjani na utakuwa  njia mbadala ya kudhibiti mapato yatokanayo na mechi.
“ Kwa mfumo huu hakuna njia ya mkato kila kitu kiko wazi na kwa kila dakika utaona mabadiliko ya idadi ya tiketi zinazonunuliwa na mpaka sasa zaidi ya tiketi 10,000 zimenunuliwa na zinazidi kununuliwa” Alisema Runyeta.
Kwa miaka mingi kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wadau wa soka nchini kuwepo kwa upotevu wa mapato katika mechi za ligi na kimataifa katika viwanja vya soka nchini kwa kuliona hilo Serikali iliamua kuanzisha mfumo utakaomaliza tatizo hilo na kukomesha mianya yote ya ulaji iliyokuwepo katika mfumo uliopita.

No comments:

Post a Comment