Sunday 25 September 2016

Mourinho na Wenger wanaelekea kufikia pabaya

Makocha hawa wawili picha haziendi kabisa na kurushiana vijembe imekuwa ni jambo la kawaida kwao.
Ni Jose Mourinho na Arsene Wenger, achana na ile ishu ya Mourinho kumwambia Wenger kwamba speshalisti wa kufeli, imefichuka kwamba Mreno huyo aliwahi kumpiga mkwara Wenger kwamba atampasua uso wake akikutana naye baada ya vita ya maneno baina yao mwaka 2014.
Bifu la Mourinho na Wenger lilirudi upya wakati Mourinho aliporejea Chelsea mwaka 2013, ambapo makocha hao kila mmoja alionyesha ubabe kwa mwenzake, ikiwamo tukio la kukunjana mashati kwenye moja ya mechi zao.
Wenger anaripotiwa kuchukizwa na Mourinho baada ya kumuuza Mhispaniola Juan Mata kwenda Manchester United na kumtuhumu kwamba anauzia maadui silaha kwa kuwa yeye ameshacheza nao. Jambo hilo liliibua malumbano na Mourinho kutoa kauli ya kumpasua Wenger.

Katika kitabu kipya cha ‘Jose Mourinho: Up Close and Personal’, kilichoandikwa na Robert Beasley, mwandishi wa habari ambaye amekuwa akifanya kazi kwa karibu sana na Mreno huyo kuna kifungu cha maneno haya yanayodaiwa ni nukuu ya Mourinho baada ya Wenger kukosoa mauzo ya Mata kwenda Man United, Mourinho alisema: “Nitamtafuta (Wenger) siku moja nje ya soka na nitampasua sura yake kabisa.

No comments:

Post a Comment