Na Rhoda Simba
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa azindua Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma leo. Anayeshuhudia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa
miaka mitano 2016/2017-2020/2021 unalenga kuboresha maisha ya Watanzania
wengi kwa kuhakikisha Sekta zinazoajiri watu wengi na walio masikini
zinakuwa kwa kasi.
Akizindua
Mpango huo leo (Jumanne, Juni 7, 2016) katika ukumbi wa Chuo cha
Mipango Mjini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali itahakikisha
Sekta za Kilimo, Viwanda, Uvuvi na Mifugo zinakua kwa kasi ya
kuridhisha ili kuongeza fursa za ajira na kupunguza umasikini. Amesema
utekelezaji wa Mpango huo ambao umefungamanisha maendeleo ya viwanda na
maendeleo ya watu na unatazamiwa kujibu changamoto ya umasikini
Tanzania.
Waziri
Mkuu amesema katika Mpango huo kuna maeneo mbalimbali ya vipaumbele
yaliyoainishwa katika Mpango huo ni miradi mikubwa kama ya chuma cha
Liganga, kufufua shirika la Ndege, Makaa ya Mawe Mchuchuma, ujenzi wa
Reli ya Kati kwa kiwango cha standard Gauge ambayo matokeo yake
yanatarajiwa kuwa kichocheo cha utekelezaji wa miradi mingine.
“Tunatarajia
ifikapo mwaka 2025 tuwe tumejenga nchi ambayo ina maisha bora, yenye
amani, umoja na utawala bora, jamii inayojifunza na iliyoelimika, yenye
uwezo wa kuzalisha na kuwa na ukuaji wa uchumi endelevu na wenye
ushindani,” amesema.
Waziri
Mkuu Majaliwa amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha ukuaji huo wa
uchumi unakuwa shirikishi zaidi katika utekelezaji wa Mpango huu na
kwamba uendelezaji wa viwanda ndio utakaoleta mafanikio makubwa karika
mwelekeo huo.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa amesema jumla ya viwanda 39 kati ya
106 vilivyobinafsishwa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambavyo
vilikuwa vya vinazalisha bidhaa za chuma, ngozi, korosho zana za kilimo,
sabuni na mafuta ya kupikia wamevifunga na kutoviendeleza.
Kufuatia
hatua hiyo Waziri Mkuu Majaliwa amesema Wizara ya Fedha na Mipango
kupitia kwa Msajili wa Hazina itaendelea na zoezi la kuvirejesha viwanda
hivyo Serikalini ili waangalie utaratibu mwingine ulio bora wa
kuviendeleza kwa kupitia Mpango huo wa Maendeleo.
Amesema
Mpango huo ambao utajikita zaidi katika kutekeleza mikakati mbalimbali
ya kuendeleza viwanda vikubwa, vya kati na vidogo na vile
vilivyobinafsishwa ili kuongeza fursa za ajira na kipato kwa wananchi
wengi.
Akizungumzia
kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka
Mitano ambao utahitimishwa Juni 30, 2016 Serikali ilifanikiwa kutekeleza
miradi ya maendeleo kama ujenzi wa barabara za lami na madaraja ya
Kigamboni, Maligisu Nagoo, Mbutu na Ruhekei. Pia ujenzi wa bomba la gesi
kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam (km 542), ujenzi wa mitambo ya
kuchakata gesi katika maeneo ya Madimba na Songosongo, ujenzi wa vituo
vya kupokelea gesi vya Somanga-Fungu na Kinyerezi.

Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wakati akizindua Mpango wa Pili wa
Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 kwenye ukumbi wa Chuo
cha Mipango mjini Dodoma Juni 7, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango kitabu cha mpango huo.
No comments:
Post a Comment