Amesema riba kubwa zinazotozwa na
baadhi ya benki, huduma zisizokidhi mahitaji na uelewa mdogo wa masuala
ya kifedha ni miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo wananchi
wanapotaka huduma za kifedha.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo
(Jumatano, Juni 15, 2016) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa
Jumuiya ya Benki za Wananchi (COBAT) mjini Dodoma.
Mkutano huo ulijumuisha wajumbe
kutoka mikoa 10 ya Kigoma, Lindi, Simiyu, Manyara, Katavi, Mbeya,
Mwanza, Morogoro, Singida na Dodoma kati ya mikoa 18 ya Tanzania Bara
ambayo bado haina Benki za Wananchi ila ipo katika hatua za kuanzisha.
Amesema changamoto nyingine ni
kutokuwepo kwa taarifa mbalimbali za sheria na taratibu ambazo
zinakwamisha ufanisi wa kiutendaji kwa baadhi ya taasisi hasa zile
zinazolenga kuwahudumia watu wa kipato cha chini.
“Tunahitaji kutafuta njia bora ya
kutatua changamoto hizi, na Benki za Wananchi ni kiungo muhimu katika
kushughulikia changamoto zinazokabili utoaji wa huduma za kifedha,”
amesema.
Waziri Mkuu amesema ni muhimu
kuanzisha Benki za Wananchi katika kila Mkoa ili kuweza kusambaza huduma
hizo karibu zaidi na walengwa, hali ambayo itasaidia kupunguza
umasikini kupitia ukuaji wa shughuli za kiuchumi.
Amesema Serikali itaangalia
uwezekano wa kuiwezesha mikoa ambayo itaonyesha ari zaidi ya kuanzisha
benki zao na akatoa wito waandae mikakati ya kuhamasisha wananchi ili
wakusanye mitaji ya kutosha.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
COBAT, Bibi Elizabeth Makwabe amesema Jumuiya yao ilianzishwa mwaka 2006
ikiwa na wanachama saba na sasa hivi wamefikia 10 huku wananchi
wanaowahudumiwa na benki hizo ni zaidi ya milioni mbili.
Amesema Jumuiya za Benki ya
Wananchi inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo mfumo hafifu wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) pamoja na ufinyu wa mitaji.
No comments:
Post a Comment