Tuesday, 14 June 2016

Wabunge 6 wakamatwa Kenya

 
Wabunge sita nchini Kenya wanatarajiwa kuwasilishwa mahakamani kufuatia madai ya kutoa matamshi ya chuki.


Siku ya Jumapili mbunge mmoja anayegemea upande wa serikali alidaiwa kutaka kuuawa kwa aliyekuwa waziri mkuu na kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga.
Wabunge wa upinzani nao pia walitoa matamshi kama hayo.
Mkuu wa idara ya jinai Ndegwa Muhoro amewaambia waandishi kwamba polisi watamkamata mtu yeyote anayeeneza matamshi ya chuki

No comments:

Post a Comment