Mwenyekiti wa chama cha mpira cha
Uingereza, Greg Dyke amewaandikia barua chama cha shirikisho la soka
barani Ulaya,UEFA kutoa maelezo ya tija kuhusu mpangilio wa ulinzi
wakati wa michuano ya soka ya Euro 2016.
Leo Urusi itacheza katika
mji wa Lile ambapo mashabiki wa Uingereza pia watakusanyika hapo kwa
kuwa mechi yao itakuwa kesho. Kulikuwa na usumbufu mkubwa katikati hapo
wakati timu zote zilipopangwa mwishoni mwa juma.Mashabiki sita wa
England wamefungwa kutokana na vurugu zilizotokea lakini hakuna yeyote
kati ya mamia ya mashabiki wa Urusi aliyewekwa hatiani,Maafisa wa Ufaransa wameliita tukio hilo kuwa ni vurugu za kihuni,hivyo timu zote mbili zilipaswa kutolewa katika michuano kama patatokea vurugu nyingine.
No comments:
Post a Comment