Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa kalenda ya msimu mpya wa mashindano na matukio ambako baada ya mapumziko ya wachazaji yanayoishia Juni 10, 2016.
Kalenda
inaonesha kipindi kinachofuata sasa ni usajili unaotarajiwa kuanza Juni
15, 2016. Usajili huo unaanza na uhamisho wa wachezaji ambako utaanza
Juni 15, 2016 hadi Julai 30, 2016.
Kwa
mujibu wa Kalenda hiyo, timu ambazo hazishiriki Ligi Kuu ya Vodacom
msimu wa 2016/2017 zitaanza kutangaza wachezaji walioachwa kuanzia Juni
15, 2016 hadi Juni 30, mwaka huu.
Kwa
upande wa timu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), watatumia
kipindi cha Juni 15, 2016 hadi Juni 30, 2016 kutangaza usitishwaji
mkataba wa wacheaji. Usajili wa utaanza Juni 15 hadi Agosti 6, kwa timu
zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Pingamizi
itakuwa ni Agosti 7 hadi 14, 2016 kabla ya kuthibitisha usajili kwa
hatua ya kwanza kati ya Agosti 15 na Agosti 19, 2016 wakati usajili
hatua ya pili utaanza Agosti 17, 2016 hadi Septemba 7, 2016 na
kitafuatiwa kipindi cha kipindi cha pingamzi hatua ya pili kuanzia
Septemba 8 hadi Septemba 14, 2016.
Septemba 15 hadi Septemba 17, 2016 itakuwa ni kipindi cha kuthibitisha usajili hatua ya pili,
Ratiba
hiyo inasema kwamba timu zinatakiwa kuandaliwa kuanzi Juni 15 2016
hadi Julai 15, 2016 ambako kuanzia Julai 16, 2016 hadi Agosti 14 ni
kipindi cha mechi za kirafiki za ndani na nje. Ratiba ya Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara itatoka kati ya Julai 16 hadi Agosti 14.
No comments:
Post a Comment