Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) kupitia Idara ya Ufundi, imetangaza kozi nne (4)
za Leseni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zinazotarajiwa kuanza Juni
20, 2016 katika mikoa ya Mwanza, Morogoro na Dar es Salaam.
Kwa
Mkoa wa Mwanza, TFF itaendesha kozi ya leseni Daraja C. kozi hiyo
inatarajiwa kuanza Juni 20, 2016 hadi Julai 4, mwaka huu ambako baadhi
ya washiriki 29 wamekwisha kujiandikisha ingawa bado kuna nafasi 11 ili
kutimiza darasa la wanafuzni 40.
Sifa za watakaochukua kozi hiyo ni kuwa kuwa na cheti ngazi ya kati (intermediate) na umahiri (activeness).
Hii ni kozi ya CAF itakayoendeshwa na TFF na kwamba watu wenye ndoto za kuwa makocha wa mpira wa miguu wanaruhusiwa kuomba.
Kwa
Jiji la Mwanza na mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa, kozi hiyo inaratibiwa
na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya TFF, Vedastus Rufano
anayepatikana kwa Namba ya simu 0753 772068 na Mwalimu atakuwa Wilfred
Kidao ambaye ni Mkufunzi wa ukocha anayetambuliwa na CAF.
Mchango kwa ajili ya mkufunzi na uendeshaji Sh. 200,000 kwa kila mwanafunzi.
Kozi nyingine ni ya leseni Daraja B
ambayo itafanyika kuanzia Julai 1, hadi Julai 16, mwaka huu mkoani
Morogoro. Kozi hiyo ambayo mchango wake ni Sh. 300,000 kwa mwanafunzi
tayari ina wanafunzi 35 na zimebaki nafasi tano tu na utaratibu wa
kuijiunga unaratibiwa na Ofisi ya Idara ya Ufundi ya TFF iliyoko Uwanja
wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Kozi nyingine ya leseni Daraja B
inaratibiwa jijini Dar es Salaam ambayo kuanzia Julai 1, hadi Julai 16,
mwaka huu ambako washiriki wa kozi hiyo ni ya TFF makocha ambao tayari
walifanya kozi ya FIFA-IOC iliyofanyika Oktoba, 2014 hivyo kwa sasa
wanatakiwa kuthibitisha kushiriki kabla ya Juni 15, 2016 katika ofisi ya
Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi.
Nafasi pia zipo kwa washiriki wengine
nje ya kundi la wale wa Oktoba, 2014 na kwamba sifa ni kuwa na Leseni
Daraja C na awe amewahi kufanya kazi ya ukocha angalau kwa mwaka mmoja
na zaidi. Mchango wa kozi hiyo ni Sh 300,000.
Kadhalika
kozi nyingine ji ya Leseni Daraja A ambayo itafanyika kuanzia Julai
17, 2016 hadi Julai 31, mwaka huu kwa hatua ya kwanza yaani Module 1
wakati Module 2 itafanyika Novemba, mwaka huu. Mchango wa kozi hiyo la
Leseni Daraja A ni Sh 600,000 ambayo inalipwa kwa pamoja.
Wakufunzi wa kozi hiyo ya juu ni
Makocha Salum Madadi na Sunday Kayuni, kabla ya CAF kumleta mtoa
tathimini ya matokeo ya makocha hao kabla ya kutoa leseni ya daraja
husika.
Washiriki wa kozi hiyo wanatarajiwa
kuwa makocha wa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
(VPL) kwani msimu wa mwisho wa makocha wa Leseni Daraja B na C ni msimu
wa 2016/2017.
Kuanzia
msimu wa 2017/2018 hakuna kocha anayeruhusiwa kuongoza timu kwa kukaa
kwenye benchi la ufundi kama hana sifa ya Daraja B na C. Msimu huu wa
2016/2017 ni nafasi ya mwisho kwa makocha wenye leseni madaraja ya chini
kukaa au kuongoza timu za zinazoshiriki VPL.
No comments:
Post a Comment