Mwanamuziki
Nyota wa Kike nchini Judith Wambura a.k.a Lady Jay Dee anayetamba na
kibao chake cha NdiNdiNdi amefanya onyesho alilolipa jina la NaamkaTenaTour katika viwanja vya Royal Village, onyesho
lililohudhuriwa na watu na watu mbalimbali akiwemo Naibu Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, Waheshimiwa
Wabunge, Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez pamoja
mashabiki wake mkoani Dodoma.
Mratibu
wa show ya Lady Jay Dee ya Naamka Tena Tour ya mjini Dodoma, Mh.
Catherine Magige akizungumza machache na kutambua uwepo wa Naibu Spika
wa Bunge na waheshimiwa wabunge wenzake katika viwanja vya Royal Village
mjini humo.
Malkia wa Bongo Flava, Lady Jay Dee katika ubora wake.
Mwanamuziki
Lady Jay Dee na The Band wakitoa burudani kwa wakazi wa Dodoma na
vitongoji vyake katika harakati za kuwafikia mashabiki wake wote nchini
nzima kwa show aliyoi' brand' kama Naamka Tena Tour.
Mkali wa R & B kwenye Band ya Lady Jay Dee, John Music akitoa burudani kwa wakazi wa Dodoma.
Vijana watanashati wa bendi Lady Jay Dee wakitoa burudani kwa mashabiki wa Dodoma.
Hoyce Temu, Esther Bulaya, Shyrose Bhanji na Hamisi Kigwangalla wakipiga shwangwe kwa Lady Jay Dee alipokuwa jukwaani.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na Naibu Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson kwenye
viwanja vya Royal Village ilipofanyika show ya mwanamuziki Lady Jay Dee
mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez (kulia) akiteta jambo na Mbunge wa
Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mh. Shyrose Bhanji kwenye show ya Lady
Jay Dee iliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mh. Esther Bulaya akiserebuka na Hoyce Temu katika show ya Lady Jay Dee iliyofanyika mwishoni mwa juma mjini Dodoma.
Mh. Halima Mdee, Mh. Catherine Magige, Mh. Esther Bulaya pamoja na Hoyce Temu wakiserebuka.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mbunge wa jimbo la
Kawe, Mh. Halima Mdee walipokutana kwenye show ya Lady Jay Dee.
Mwanamuziki Lady Jay Dee na Band yake wakishambulia jukwaa.
Mashabiki wa Lady Jay Dee wakiserebuka kwa raha zao.
Pichani
juu na chini ni Umati wa wakazi wa mjini Dodoma eneo la VIP wakiwemo
waheshemiwa wabunge wakisakata muziki wa Lady Jay Dee.
Upendo waliounyesha watu wa Dodoma kwa mwanamuziki Lady Jay Dee.
No comments:
Post a Comment