Rais wa Marekani Barack Obama
ametangaza kumuunga mkono Hillary Clinton kuwa mgombea urais wa chama
cha Democratic katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu
nchini Marekani.
Amechukua hatua hiyo muda mfupi baada ya kukutana na seneta wa
Vermont Bernie Sanders ambaye amekuwa akikabiliana na Bi Clinton katika
kinyang’anyiro cha kumchagua mgombea wa chama hichoAkizungumza kwenye video ambayo imewekwa kwenye Twitter na Bi Clinton, Bw Obama amesema mgombea huyo ndiye aliyewahi kuhitimu zaidi kuwa rais wa Marekani.
“Niko pamoja naye, nina msisimko na nasubiri sana kutoka huko nje na kufanya kampeni na Hillary,” amesema Obama.
No comments:
Post a Comment