Picha na Ally Daud-Maelezo
Na Ally Daud- Maelezo
Rais mstaafu wa awamu ya tatu
Mhe.Benjamin William Mkapa amewataka watanzania kuunga mkono juhudi za
Serikali ya awamu ya tano kwa kufanya kazi kwa bidii na kupunguza
lawama ili kuonyesha uzalendo aliouacha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere.
Rais Huyo Mstaafu ameyasema hayo
katika mkutano wa nane wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere ambao umefanyika
katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu Cha Dar es salaam na kuongeza kuwa
watanzania wengi wamekua na desturi ya kutumia muda mwingi Katika
kuilaumu serikali baada ya kufanya kazi kwa maendeleo ya nchi.
“Watanzania tunatakiwa tufanye
kazi kwa bidii ili tuifikishe nchi yetu Kwenye maendeleo na si kutumia
muda mwingi Katika kuilaumu serikali ” alisema Dkt Mkapa.
Aidha Dkt. Mkapa amesema kuwa ili
uzalendo uwepo tunatakiwa kutumia vizuri uhuru wa kuongea Katika kuleta
maendeleo na si kuleta uchochezi Katika nchi na kusababisha uvunjifu wa
amani ambayo ameiacha Mwal. J.k nyerere.
Mbali na mkutano huo pia kulikua
na uzinduzi wa kitabu cha uchumi wa kisiasa wa madiliko ya Tanzania
kijulikanacho kama (political economy of change in Tanzania) ambacho
kina lengo la kukuza uchumi na siasa nchini.
Mkutano huo wenye lengo la
kudumisha uzalendo na kukuza uchumi nchini umeudhuriwa na wawakilishi
Mbali Mbali wa kitaifa na kimataifa wakiwemo baadhi ya mabalozi na
wanazuoni kutoka ndan na nje ya nchi.
Kwa upande wa Makamu mkuu wa Chuo
Kikuu Cha Dar es salaam Prof. Rwekaza Mukandala alisema kuwa mkutano
huo unalenga kudumisha na kuendeleza aliyoyaacha Baba wa Taifa Hayati
Mwl. J.k Nyerere.
Mbali na hayo amewataka vijana na
watanzania kwa ujumla kumuenzi kwa kufanya kazi kwa bidii ili
kujikwamua kiuchumi na kuendeleza ujamaa aliouacha Mwalimu.
No comments:
Post a Comment