Timu ya Taifa ya vijana chini ya
miaka 17 (Serengeti Boys) kinaingia kambini leo Juni 14, 2016 kujiandaa
na mchezo wa kufuzu fainali za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi
ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.
Makipa:
- Kelvin Deogratius Kayego,
- Ramadhani Awm Kambwili na
- Samwel Edward Brazio.
Mebeki wa Pembeni:
- Kibwana Ally Shomari,
- Israel Patrick Mwenda,
- Anton Shilole Makunga na
- Nickson Clement Kibabage.
Mabeki wa Kati:
- Dickson Nickson Job
- Ally Hussein Msengi na
- Issa Abdi Makamba
Viungo wa Kuzuia:
- Kelvin Nashon Naftal
- Ally Hamis Ng’anzi na
- Shaban Zuberi Ada
Mawinga:
- Mustapha Yusuph Mwendo
- Yassin Muhidini Mohammed
- Syprian Benedictor Mtesigwa na
- Gadafi Ramadhan Said
Viungo wa kushambulia:
- Asad Ali Juma
- Mohammed Abdallah Rashid na
- Muhsin Malima Makame
Washambuliaji:
- Ibrahim Abdallah Ali
- Enrick Vitaris Nkosi
- Rashid Mohammed Chambo na
- Yohana Oscar Mkomola
Katika kuajindaa na mchezo huo,
Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya
vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth
Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu
katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Kadhalika Serengeti Boys ilicheza
mfululizo michezo saba ya kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri (2),
India, Korea Kusini, Malaysia na Marekani (USA). Kabla ya hapo timu hiyo
ilicheza michezo kadhaa ya ndani na timu za chini ya umri wa miaka 20
bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Katika mashindano ya AIFF, timu
hiyo pekee kutoka Afrika na ambayo ilikua kipenzi cha mashabiki katika
jiji la Goha ilicheza na timu ambazo ziko juu katika hatua za juu katika
mtoano wa kuwania kushiriki Kombe la Dunia kupitia mabara yao yaani
CONCACAF (USA) na AFC (India, Korea na Malaysia).
VIWANJA LIGI KUU YA VODACOM NA DARAJA LA KWANZA
Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), limetoa taarifa kwa barua kwa timu zote zitakazoshiriki Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Ligi daraja la Kwanza ya StarTimes kwa
msimu wa 2016/17 kwamba kila timu imetakiwa kuwasilisha jina la Uwanja
ambao utatumia kama uwanja wa nyumbani kabla ya Juni 20, 2016.
Barua hiyo iliyotumwa kupitia Bodi ya Ligi (TPLB) ya TFF imeagiza jina la uwanja huo uende sambamba na taarifa za:
– Vipimo vya uwanja
– Iwapo unaweza kutumika kwa mechi za usiku au la
– Idadi ya vyumba vya kubadilishia nguo ‘dressing rooms’
– Uwezo wa uwanja kuingiza mashabiki
– Mmiliki wa uwanja huo
– Aina ya nyasi (asili au bandia)
Tumezielekeza kwamba iwapo timu
haina uwanja wa nyumbani unaofaa kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom
inaweza kuchagua uwanja mwingine katika mji au mkoa wa jirani. Hii ni
kwa mujibu wa Kanuni ya 6 (3) Ligi Kuu Tanzania Bara toleo la 2016/17.
Tayari TFF, limetoa kalenda ya
msimu mpya wa mashindano na matukio ambako usajili kuanza Juni 15, 2016.
Usajili huo unaanza na uhamisho wa wachezaji ambako utaanza Juni 15,
2016 hadi Julai 30, 2016.
Kwa mujibu wa Kalenda hiyo, timu
ambazo hazishiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 zitaanza
kutangaza wachezaji walioachwa kuanzia Juni 15, 2016 hadi Juni 30, mwaka
huu
.
Kwa upande wa timu
zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), watatumia kipindi cha Juni
15, 2016 hadi Juni 30, 2016 kutangaza usitishwaji mkataba wa wacheaji.
Usajili wa utaanza Juni 15 hadi Agosti 6, kwa timu zinazoshiriki Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Pingamizi itakuwa ni Agosti 7
hadi 14, 2016 kabla ya kuthibitisha usajili kwa hatua ya kwanza kati ya
Agosti 15 na Agosti 19, 2016 wakati usajili hatua ya pili utaanza Agosti
17, 2016 hadi Septemba 7, 2016 na kitafuatiwa kipindi cha kipindi cha
pingamzi hatua ya pili kuanzia Septemba 8 hadi Septemba 14, 2016.
Septemba 15 hadi Septemba 17, 2016 itakuwa ni kipindi cha kuthibitisha usajili hatua ya pili,
Ratiba hiyo inasema kwamba timu
zinatakiwa kuandaliwa kuanzi Juni 15 2016 hadi Julai 15, 2016 ambako
kuanzia Julai 16, 2016 hadi Agosti 14 ni kipindi cha mechi za kirafiki
za ndani na nje. Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itatoka
kati ya Julai 16 hadi Agosti 14.
No comments:
Post a Comment