Wednesday, 15 June 2016

Mkutano wa kusikiliza maoni kuhusu mswada wa fedha wa mwaka 2016


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa mujibu wa Kanuni ya 118 ya Kanuni za
Kudumu za Bunge, Toleo la mwaka 2016, Nyongeza ya Nane, Sehemu ya Tatu Kifungu
cha 9, imepewa jukumu la kusikiliza maoni na mapendekezo ya wadau kuhusu
Muswada wa Sheria ya Fedha kila mwaka.
 

Katika kutekeleza jukumu hilo, Kamati ya Bajeti imepanga kufanya Mkutano wa Wadau
wote wa masuala ya kodi (Public Hearing) kwa ajili ya kusikiliza maoni yao na
mapendekezo kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2016.

Mkutano huo umepangwa kufanyika siku ya Alhamisi Tarehe 16 Juni 2016 kuanzia Saa
Tano asubuhi katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Mkoani Dodoma.
Kwa kuzingatia umuhimu wa Muswada huo, Kamati inawaalika wadau wote kufika na
kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa katika hatua nyingine. Maoni ya wadau
yanaweza pia kuwasilishwa kwa njia ya Posta au Barua pepe kwa anuani ifuatayo:
Katibu wa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 941,
DODOMA
Imetolewa na,
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano.
Ofisi ya Bunge,

No comments:

Post a Comment