Wednesday, 15 June 2016

Jinsi amani inavyotoweka na shughuli za maendeleo zinaposimama

Amani ni msingi wa maendeleo na hivyo ni muhimu kwa nchi yoyote duniani.Bila amani,nchi haiwezi kufanya shughuli za maendeleo hata pale ambapo maendeleo yameshapatikana,yanaweza kuvurugwa endapo amani itatoweke katika nchi.

Nchi  ambazo kwa miaka ya hivi karibuni zimejitahidi kupiga hatua za maendeleo na zinaendelea kufanya jitiada kuhakikisha kuwa zinapiga hatua kubwa zaidi ya maendeleo kwa faida ya wananchi wote,jitiada hizo pia,kwa baadhi ya nchi zimeathiriwa na migogoro.

Matokeo ya migogoro hiyo ni mamilioni ya waafrika wasio na hatia kupoteza maisha yao na mamilioni zaidi kujeruhiwa.Pia mamilioni ya wanawake na watoto kupatwa shida kubwa na baadhi ya watu kukimbia nchi zao na kukimbilia nchi za jirani katika kuokoa maisha yao hivyo kujikuta wakiishi maisha ya dhiki nje ya nchi yao.

Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2009,Afrika ilikuwa na wakimbizi milioni 3 ambayo ni asilimia 20 ya wakimbizi wapatao milioni 10.5 duniani.Aidha,Afrika inakisiwa kuwa ina watu milioni kumi na mojana laki sita ambao wamelezimika kuhama makazi yao kwa ajili ya vita
Migogoro migogoro huwa kikwazo kikubwa cha shughuli za maendeleo siyo tu kwa watu binafsi bali pia kwa taifa.Fedha ambazo zingeweza kuelekezwa kwenye huduma muhimu ya jamii kama afya,elimu,maji ni fedha ambazo huelekezwa katika manunuzi ya silaa.

Inakadiriwa kuwa hasara ya kiuchumi inakadiriwa kuwa wastani wa dola bilioni kumi na nane kwa kila mwaka sababu ya migogoro.

Hali hii ya migogoro katika bara la Afrika imelifanya  bara hili kujulikana kama bara la mapigano jambo ambalo ni dhahiri linasikitisha hivyo hatuna budi kuondokana na hali hiyo ya migogoro na kuwa bara huru lisilo na migogoro.

Ni kweli kuwa katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mabadiliko,kutokana na juhudi zilizofanyika,Afrika imefanikiwa kupunguza idadi ya migogoro kuliko ilivyokuwa katika miaka ya 1980 wakati ambapo nchi nyingi zilikuwa na migogoro

Mfano nhci kama Liberia,Sierra Leone,Msumbiji,Angolo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),Burundi na Comoro nazo zimeendelea kuimarisha amani,Hali hii inatupa faraja lakini bado Bara la Afrika linamigogoro kama vile ya Somalia na Darfur kuko Sudani.

Mgogoro wa Somalia ni mgogoro wa muda mrefu sasa ambao ni changamoto kubwa kwa bara la Afrika na jamii ya Kimataifa kwa ujumla na hivyo unahitaji kuangaliwa kwa umakini zaidi.
Hali ya usalama nchini Somalia ambayo kwa takribani miaka ishirini sasa imekuwa katika mazingira ya kusikitisha kwa takribani miaka ishirini sasa imekuwa katika mazingira ya kusikitisha ambapo kwa ujumla usalama wa wananchi wan chi hiyo umo katika hali ya hatihati.
Kwa upande Tanzania tunafahari kubwa ya kuwa mstari wa mbele katika kujenga mazingira yetu wenyewe ya kuwa na amani,utulivu na mshikamano na pia katika kusaidia ndugu na majirani zetu na sehemu nyingine za Bara la Afrika katika kufanukisha lengo la kuleta amani popote pale inapokosekana.

Sote tunatambua kuwa Serikali ya Tanzania katika kutetea amani katika bara la Afrika imepeleka vijana wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) katika miaka ya nyuma walikwenda nchini Liberia kwa lengo hilo.Na hivi karibuni wanajeshi wetu wamekwenda Darfur kuungana na wanajeshi wengine wa Kiafrika na nchi nyingine chini ya uongozi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment