Thursday 23 April 2015

Simba yazinduka kwa Mgambo


Kikosi cha Simba 2015.
SIMBA jana ilizinduka na kuifunga Mgambo Shooting mabao 4-0 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Bao la kwanza la Simba lilifungwa na Emmanuel Okwi katika dakika ya nane baada ya kuunganisha pasi ya Ramadhan Singano. Singano aliifungia Simba bao la pili katika dakika ya 15 baada ya kupiga mpira wa kona uliokwenda moja moja kutikiza nyavu za Mgambo.
Katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo Simba ndio ilitawala zaidi na mchezaji wake Ibrahim Ajibu alipoteza nafasi ya wazi katika dakika ya 19 baada ya shuti lake kupanguliwa na kipa wa Mgambo Godson Mmasa.

Dakika ya 42 Okwi aliongeza bao la tatu kwa Simba baada ya kutumia vema makosa ya mabeki wa Mgambo Bashiru Chanache na Salim Kipanga.
Okwi ambaye alikuwa mwiba mchungu kwa Mgambo jana alifunga bao la nne katika dakika ya 50 baada ya kupokea pasi ya Ajibu kabla ya kumlamba chenga kipa wa Mgambo.

No comments:

Post a Comment