Friday 10 April 2015

mgomo wa mabasi Tanzania serikali mupo wapi?


 




Mtwara Magari hayakutoka kwenda Dar kwasababu hawajui hatma ya huko Dar ila walikuwa tayari kusafieisha abiria, daladala na magari ya wilayani hakuna.

=> Kuna magari yamezuiwa Chalinze, wamepewa taarifa kuwa waliotangulia mbele Chalinze wamepigwa mawe.

=> Hapa stendi ya Njombe mabasi hayajaondoka mpaka muda huu.

=> Kuna zaidi ya mabasi zaidi ya 15 kutoka kanda ya ziwa, yamezuiwa/yamekwama Wilaya ya Kibaha, wamepewa taarifa kuwa waliotangulia mbele ya Chalinze wamepigwa mawe. Wanahofia Vurugu zinazo endelea Dar es Salaam

=> Hapa Tabora, mabasi ya kwenda mikoani mpaka sasa abiria hawajui mustakabali wa safari

=> Hapa Mbagala Rangi 3, kuna baadhi ya daladala zimeamua kuendelea kuchukua abiria lkn zinavamiwa na madereva wanaoshinikiza mgomo. Wanawashusha abiria toka kwenye daladala
 

No comments:

Post a Comment