Sunday 12 April 2015

AJALI YA LORI NA BASI LA ABIRIA RUAHA MBUYUNI LEO



Wimbi la ajali limeendelea kuitikisa nchi baada a ajali nyingine mbaya kutokea leo hii asubuhi maeneo ya Ruaha Mbuyuni ikihusisha basi la Nganga linalofanya safari zake kati ya Iringa na Kilombero na gari aina ya Fuso kugongana uso kwa uso na kisha magari yote kushika moto. Kwa mujibu wa mtoa habari idadi kubwa ya abiria wamepoteza maisha kwa kuteketea kwa moto na wengine ni majeruhi. Jeshi la Polisi linaenelea na uchunguzi wa chanzo cha habari hiyo. Pichani ni magari aliyohusika na ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment