Sunday 12 April 2015

Tanesco yasema hakuna mgao wa umeme kama taarifa zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari.


Mkurugenzi mkuu wa shirika la umeme nchini Tanesco Bwana Felchesmi Mramba amesema hakuna mgamo wa umeme kama taarifa zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kwa muda siku tisa kutokana na kuendelea kwa matengenezo ya mtambo wa Songosongo na badala yake shirika hilo limebuni mbinu mpya ya kuendelea kusambaza umeme kama kawaida kwa wateja wake licha ya mitambo hiyo kuendelea kufanyiwa marekebisho ya kiufundi. 
Kuhusu kukatika kwa umeme mara kwa mara kwa baadhi ya maeneo hapa nchini Bwana Mramba amesema hali hiyo imetokana na miundombinu ya shirika hilo kuharibika kipindi mvua zinaponyesha hivyo kusababisha umeme kukatika baada ya kuharibika na sio mgao.

No comments:

Post a Comment