Sunday 12 April 2015

Wakimbizi wa Somalia:UN yaijibu Kenya


Kambi ya wakimbizi wa Somalia ya Daadab
Umoja wa mataifa unasema kuwa haujapokea amri rasmi kutoka kwa serikali ya Kenya ya kuutaka ufunge kambi ya wakimbizi ambayo ni makao kwa maelfu ya raia wa Somalia.
Siku ya jumamosi makamu wa rais wa Kenya William Ruto alisema kuwa amelipa shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa mataifa muda wa miezi mitatu ya kufunga kambi hiyo na kuwasafirisha wakimbizi hao kwenda nchini Somalia.
Amesema kuwa la sivyo Kenya itachukua jukumu hilo mikononi mwake.
Baadhi ya wanasiasa nchini Kenya wanaamini kuwa kambi hiyo imekuwa eneo la kuwapa mafunzo wanamgambo wa Al shabaab ambao waliwaua karibu wanafunzi 150 wa chuo cha Garissa zaidi ya wiki moja iliyopita

No comments:

Post a Comment